IEBC Yamchunguza Gavana Ranguma Kwa Madai ya Kutumia Nembo Za ODM

Tume Huru ya IEBC imeanzisha uchunguzi dhidi ya gavana wa Kisumu Jack Ranguma, kufuatia madai ya kutumia rangi za chama cha ODM na Muungano wa National Super Alliance - NASA kwenye mabango yake ya kampeni, licha ya kuwa mgombea huru.

Afisa mkuu wa IEBC katika kaunti ya Kisumu John Lorionokou, amesema watachukua hatua mwafaka baada ya uchunguzi huo.Viongozi wanaoegemea chama cha ODM katika kaunti ya Kisumu, wakiongozwa na mbunge wa Nyando Fred Otieno Outa, wamemkosoa gavana Ranguma kwa madai ya kutumia rangi na nembo za chama hicho cha chungwa.

Viongozi wanaoegemea chama cha ODM katika kaunti ya Kisumu, wakiongozwa na mbunge wa Nyando Fred Otieno Outa, wamemkosoa gavana Ranguma kwa madai ya kutumia rangi na nembo za chama hicho cha chungwa.

Hata hivyo, Gavana Ranguma amepuuzilia mbali madai hayo.

Ranguma anawania ugavana kama mgombea huru, baada ya kushindwa na Seneta wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyong’o, kwenye mchujo wa chama cha ODM mapema mwaka huu.