PATANISHO: Nililala Na Mpenzi Wa Ndugu Yangu Nikiwa Mlevi

Edwin aliwashangaza wengi alipotuma ujumbe akitaka apatanishwe na nduguye, Felix ambaye alilala na bibi yake akiwa amelewa chakari.

"Sasa ndugu yangu Felix alikuwa na msichana ambaye sio bibi yake lakini mpenzi wake na walikuwa wamejuana kwa mwezi mmoja. Sasa kuna wakati walikuwa wanataka kwenda Bungoma kwetu nyumbani na Felix alikuwa Mombasa lakini mwanadada alikuwa Nairobi.

Hapo Felix alimueleza atangulie safarini kwani angekuja amchukue kwangu Nakuru. Sasa mwanadada alifika saa tatu usiku na hiyo siku ilikuwa Jumamosi na nilikuwa nimelewa, alipokuja nikampokea vizuri. Sasa alipokula akanieleza kuwa pia yeye hunywa pombe na akanieleza nimwekee. Sasa nikamueleza atakapolala ikifika wakati wa kulala.

Alikuja kwa chumba changu na tukalala lakini sikumbuki tukifanya chochote kwani asubuhi nikiamka alikuwa kando yangu. Felix alikuja kesho yake kama saa tisa na wakaanza safari mda wa saa moja. Baada ya wiki tatu hivi ndugu yangu alinipigia akidai kuwa tunafaa kuzungumza kwani mpenzi wake alimueleza kuwa nililala naye." Alijieleza Edwin akidai kisa hicho kilitokea mwezi mmoja uliopita.

Alipopigiwa simu Felix, "Huyu jamaa nilikuwa nasafiri kwenda Bungoma na mpenzi wangu alikuwa Nakuru na nikamueleza apitie kwa ndugu yangu Nairobi na sijui nini ilitokea. Huyu msichana akazusha akidai vile walilala na ndugu yangu. Sasa tulikosania mambo ya nyumba na akaropokwa sasa nilimpiga sana na tukaachana." Alijieleza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be