Ndugu Watatu Wafariki Huko Bungoma Baada Ya Mzozo Wa Shamba

Watu watatu kutoka kijiji cha Luanda B Eneo bunge la Tongaren huko Bungoma wameaga dunia baada ya kunyongwa, kupigwa na kuteketezwa kutokana na mzozo wa kipande cha ardhi.

Jamaa wa kwanza anadaiwa kunyongwa na kaka zake jambo lililowapandisha wenyeji mori na kuwaua washukiwa wawili kabla ya kuteketeza miili yao.

Inadaiwa mshukiwa mkuu Sammy Simiyu alitaka kuuza kipande cha ardhi cha familia anunue pikipiki japo nduguye alipinga hapo aliamua kumuua kakake kwa ushirikiano na washukuwa wengine watatu.

Miili yao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Kiminini nursing home huku polisi wakianzisha uchunguzi zaidi juu ya kisa hicho.

-Brian Ojamaa