Mabadiliko katika baraza la mawaziri

kanzedenaatstatehpuse
kanzedenaatstatehpuse
Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa alasiri amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na kuteua mabalozi wapya, hii ikiwa ni mojawapo wa juhudi zake za kuimarisha Serikali kuambatana na  nguzo nne za ajenda yake ya Maendeleo.

Baraza la Mawaziri

1. Waziri Aden Mohammed amehamishwa na kupelekwa katika Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ustawi wa Kandaa katika wadhifa huo huo.

2. Naye Peter Munya ndiye Waziri Mpya wa Ustawi wa Viwanda, Biashara na Vyama vya Ushirika .

3. Professa Collete Suda amehamishwa kwenda katika Wizara ya Elimu kama Msimamizi Mkuu na vile vile Katibu katika Idara ya Elimu ya Vyuo Vikuu.

4. Bw. Simon Kachapin amehamishwa kwenda Wizara ya Kawi kama Msimamizi Mkuu.

Makatibu wa Wizara

5. Katibu Mkuu Charles Sunkuli amehamishwa kutekeleza wadhifa huo huo katika Idara ya Ugatuzi;

6. Katibu Mkuu Nelson Marwa amehamishwa kutekeleza wadhifa huo huo katika Idara ya Masuala ya Kijamii, Penisheni na ya Wazee;

7. Katibu Mkuu Zainab Abdalla Hussein amehamishwa kwenda katika Idara ya Urekebbishaji wa tabia;

8. Katibu Mkuu Alfred Cheruiyot amehamishwa kwenda katika Idara ya Ustawi wa Mafunzo ya Kazi za Ufundi;

9. Katibu Susan Mochache amehamishwa kwenda katika Idara ya Ustawi wa Mazingira na Misitu ;

10. Bw. Joe Okudo ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Idara ya Utalii;

11. Dkt. Margaret Mwakima sasa ndiye Katibu Mkuu katika Idara ya Hifadhi za Wanyama Pori;

12. Dkt. Ibrahim A. Mohammed ameteuliwa Katibu Mkuu katika Idara ya Ustawi wa Wafanyakazi.

13. Bi. Fatuma Hirsi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Idara ya Utangazaji na Mawasiliano ya Simu ;

14. Prof. Micheni Japheth Ntiba amehamishwa kuwa Katibu Mkuu wa Idara ya  Ustawi wa Uvuvi, Viumbe vya Majini na  Uchumi wa Raslimali za Baharini .

Mabalozi

Wafuatao wameteuliwa kuwa mabalozi endapo wataidhinishwa na bunge:

15. Bi. Sarah Serem

16. Luteni  Jenerali Samuel Thuita

17. Bw. Francis Muhoro

18. Bw. Manoah Esipisu

19. Bw. Paddy Ahenda

20. Balozi. Peter Nicholas Oginga Ogego

21. Johnson Kimani Ondieki

22. Chris Karumba Mburu

23. Mheshimiwa Benjamin Langat