Patanisho: Mke wangu alitoweka nyumbani nilipo safiri kikazi

George aliomba apatanishwe na mkewe aliyetoka miezi miwili bila wao kukosana. Aliongeza kuwa hapo juzi alimtusi baada yake kumdanganya mara kadhaa kuwa atarudi nyumbani.

"Amekuwa akinisumbua na kunidanganya sasa nikakasirika na nikamtusi. Tumeoana kwa miaka minane na nilimuoa nikiwa na umri wa miaka ishirini." Alieleza.

Nilitoka nikielekea kazini ukambani na nikamuachia fedha za kutumia kwani nilikuwa nasafiri kwa siku nne. Dadangu alikuwa kwa nyumba na watoto wawili, kufika kumpigia mke wangu simu kumueleza nimefika hakujibu simu. Kupigia dadangu akadai mke wangu hakurudi aliponizindikiza.

Jirani yangu ndio alinieleza kuwa alimuona mke wangu na begi kubwa lakini kumuuliza mke wangu alikuwa ananidanganya yuko nyumbani." Aliongeza huku akidai mkewe alidai kuwa alikuwa ameenda kumuona daktari kwani ana shida ya kutozaa.

Kumtumia nauli hakurudi, aka block simu yangu na nikimpigia akiskia sauti yangu anazima simu.

Quinta alipopigiwa simu alisema kuwa atarudi nyumbani Jumatatu ijayo.

&feature=youtu.be