Wakenya waungana na KWS kusherehekea siku ya fisi duniani kwa jumbe za kuchekesha

“Je, wale wa kina 'Kevo' wamejumuishwa? sababu nina rafiki na tunahitaji sababu ya kusherehekea" Mmoja aliuliza huku mwingine akifananisha kicheko cha fisi na wanasiasa.

Muhtasari

• Wakenya, kwa ucheshi wao, walifurika kwenye kutoa maoni na kuandika jumbe za kuchekesha kuhusu mnyama fisi

SIKU YA FISI DUNIANI
SIKU YA FISI DUNIANI
Image: X//KWS

Aprili 27, Shirika la wanyamapori la Kenya liiungana na wapenzi wa wanyamapori duniani kusherehekea siku ya fisi duniani.

Kupitia ukurasa rasmi wa X, KWS walichapisha picha ya fisi na kufichua kwamba ni mnyama mwenye umuhimu mkubwa katika maisha ya pori, huku wakiomba Wakenya kujiunga nao katika kuashimisha siku hiyo spesheli kwa ajili ya mnyama huyo asiyependwa na binadamu.

“Leo ni Siku ya Kimataifa ya Fisi! Wacha tusherehekee jukumu muhimu la fisi katika kudumisha mfumo wa ikolojia. Kwa kuguguna mifupa, wao husafisha mazingira, kuzuia kuenea kwa magonjwa na kukuza maelewano ya kiikolojia, na hivyo kuhakikisha makazi yenye afya kwa spishi zote. Je, ni mambo gani mengine unayofahamu kuhusu fisi?” KWS waliuliza kwenye X.

Wakenya, kwa ucheshi wao, walifurika kwenye kutoa maoni na kuandika jumbe za kuchekesha kuhusu mnyama fisi, wengine wakitania tahadhari ya awali ya KWS kuwa ukimuona fisi hufai kutoroka bali unafaa kusimama na kuzungumza naye.

Hizi hapa ni baadhi ya jumbe za kuchekesha kutoka kwa Wakenya kwenye mtandao wa X;

“Fisi ni wawindaji stadi, wanaoweza kukamata mawindo makubwa kama nyumbu na pundamilia. Walakini, mara nyingi wanaonyeshwa kwa njia isiyo ya haki kama waporaji tu. Fisi wana mlio wa kitabia wa "kucheka" ambao unaweza kusikika umbali wa kilomita 5,” Fisi African Safaris walisema.

“Kwa kifupi leo ni siku ya wanaume duniani, semeni hivyo” Rambo Kanambo alisema.

“Je, wale wa kina 'Kevo' wamejumuishwa? sababu nina rafiki na tunahitaji sababu ya kusherehekea” Kenay Bett.

“Fisi wana kicheko cha kupendeza na kunikumbusha wanasiasa” Mary Hairy.

“Watu wa Juja wamekuwa wakiwapigia kelele Fisi” Okonjo.

Maoni yako ni yepi kuhusu fisi?