Jambo Massawe: Bwanangu alinipea notice nihame

massawe international women's
massawe international women's
Bi Lydiah alishangaza huku akiwachekesha wengi aliposimulia jinsi mumewe alivyompa notisi ya kuhama kwa nyumba yao baada yake kusafiri kwenda mashambani.

Kulingana na Lydiah, wawili hao walisafiri kwenda kumzika mamake na basi alipotaka kurudi kuwasalimia jamaa zake baada ya siku arobaini, mumewe hakufurahishwa na hayo.

Licha ya bwanake kutowajibika nyumbani, Lydiah alipewa notisi kuhama kwake baada ya kurudi kutoka mashambani.

Pata usimulizi wake.

Imagine, mimi ndio nagharamia kila kitu lakini maajabu nimepewa notice na bwanangu akiniambia nijipange nitoke. Sijafanya chochote baada ya ndoa ya miaka kumi na moja akisema amechoka nami.

Nilienda mazishi ya mamangu na hakufurahia niliporudi. Alikuja mazishi na unajua after 40 days nikarudi nyumbani kutembea pamoja na jamii yangu, na hakupendezwa na hayo. Wakati wa kurudi nyumbani akanitumia ujumbe akiniambia nijipange.

Sasa nilikuwa nataka kujipanga kivyangu nijue nitakavyo ishi na watoto wangu. Imagine ananipa notice na mimi ndio nanunua kila kitu kwa nyumba, isitoshe akipata pesa huanza kelele kwa nyumba ili nisimuitishe chochote.  

Skiza uhondo.

&feature=youtu.be