PATANISHO: Niliogopa kuwa mume wangu anaweza niua

Patrick alituma ujumbe akiomba kupatanishwe na mkewe Sylvia, mwenye umri wa miakaa 28, mbaye alipata amefunganya virago vyake na kuondoka mwezi wa Disemba tarehe 30.

Kuna kijana fulani ambaye alikuwa anamtaka na mimi kuja kugundua hayo maneno, kumuuliza ikawa tunakosana naye na baadae akaja akaniambia huyu kijana alikuwa anamtaka, lakini alimueleza kuwa yeye ni mpwa wake na hawawezi pelekana mahali. Alijieleza Patrick.

Sasa nikamweleza kuwa sikuwa naelewa hayo maneno na sasa kwa ajili nimeelewa basi hayo maneno tuyaache. Na hapo baadae akanitumia ujumbe akisema nimsamehea maneno yote aliyonifanyia.

Nikamwambia nishamsamehe na tuishi na amani, sikujua on Sunday nikitoka kazini nitamkosa. Nilipata amekusanya vitu vyake na ameenda huku watoto akiwa amewapeleka kwa mamake. Aliongeza akidai kuwa hajui kwenye mkewe aliko kwani alimwambia yuko Naivasha.

Kulingana na Patrick 31, wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano lakini bado hawajaona ki rasmi.

Unajua Gidi wacha nikuambie, mapenzi inakuanga ya watu wawili lakini mtu wa tatu, nne akiingia inakuwa tu hivo. Kwa hivyo mimi niliboeka. Alisimulia Sylvia.

Mimi niligundua kuwa tukivuruga kidogo yeye huenda kuambia ndugu zake mpaka anaingiza wazazi wake na tukimaliza maneno, hatukai hata wiki moja kabla ya kurudisha yale maneno. 

So niliona hakuna haja ya kuendelea na yeye, unajua mtu anaweza kuambia amekusamehe na kwa roho hajakusamehe. Mimi niliogopa kwani mtu hata anaweza kuua. Aliongeza.

Pata uhondo kamili.