Rais Uhuru Kenyatta apokea risala za rambirambi na heri njema kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari

Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi, alipokea risala ya rambirambi na  ya heri njema kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria kufuatia shambulizi la kigaidi wiki hii katika mtaa wa Riverside Drive lililosababisha maafa ya watu 21 na kadhaa kujeruhiwa.

Risala hiyo ya rambirambi na ya heri njema iliwasilishwa na ujumbe ulioongozwa na mjumbe maalumu Profesa Ibrahim Agboola.

Mfanyi biashara Alhaji Mohammed Indimi aliyendamana na Mjumbe huyo maalum pamoja na Balozi wa Nigeria hapa nchini Balozi Shiedu Omeiza Momoh walimpongeza Rais Kenyatta kwa juhudi zake za kuhakikisha mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini Kenya.

Katibu Katibu katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni Balozi Macharia Kamau alihidhuria hafla hiyo.