Mwanafunzi aliyezuiliwa kuingia Starehe ajiunga na Mang'u

Baada ya shule ya upili ya starehe mapema wiki jana kumkataza Jack Mbabu kujisajilli au kuwa mwanafunzi wa shule hiyo, sasa apata uandikishaji wa shule ya upili ya Mang'u.

Mvulana huyo alipata alama 417 katika mtahani wake wa darasa la nane (K.C.P.E).S tarehe walimkataza mwanafunzi huyo wakisema kuwa baba yake alikuwa jeuri ama alikuwa hana nidhamu yeyote kwa shule hiyo.

Vilevile, hawakukamilisha kujaza kartasi za uandikishaji wa hiyo shule huku ikimbidi waziri wa elimu Amina kumteulia shule ya upili ya Mang'u.

Ndoto za Jack hazikuambulia patupu bali aliweza kuteuliwa shule nyingine ili kukamilisha ndoto zake za maisha. Baadaye huduma ya masomo nchini ilimpa jack mbabu msaada wa haraka wa uandikishaji wa shule ya upili ya Mang'u.

Mbunge wa Imenti kusini Kathuri Murungi aliweza kusambaza habari hizo na kusema "Tuna hukumu shule ya upili ya starehe kwa kushindwa kumuandikisha jack japokuwa alikuwa na ruhusa kutoka (Nemis) kujiunga na shule hiyo.

"Hakuna sababu yeyote ambayo wangekataa kumuandikisha mwanafunzi huyo, uchunguzi unapaswa kufanywa, na kamati ya bunge ya elimu inapaswa kufuatilia jambo hilo na kumualika mkurugenzi wa shule hiyo kuelezea kamati sababu zilizofanya shule kumkataa Jack Mbabu."

Amina Mohammed aliweza kusema mwanafunzi huyo aweze kupata nafasi katika shule ya Mang'u haraka iwezekanavyo.

"Suala hlo limetatuliwa na mwanafunzi huyo mwenye alikuwa aende shule ya Starehe amepelekwa shule ya upili ya Mang'u.

-The Star