Mauaji: Bawabu mmoja kuuwawa na majambazi kaunti ya Makueni

0fgjhs21ivvmeida3g.6c5484c4(2)
0fgjhs21ivvmeida3g.6c5484c4(2)
Bawabu mmoja wa eneo la burudani huko Kambu, kaunti ya Makueni ameuliwa baadaya ya majambazi waliojihami kwa silaha butu kuvamia klabu hicho alfajiri ya leo.

OCPD wa Kibwezi Ben Changulo anasema majambazi hao ambao walimjeruhi pia meneja wa kilabu hicho walifanikiwa kuiba shilingi elfu mbili pamoja na mali nyingine.

"Ilikuwa saa kumi na moja ambapo watu waliingia wakiwa wamejihami, wakamjeruhi maneja wa klabu hicho kisha kumuuwa bawabu," Alielezea Ben.
Polisi tayari wameanza msako kuwakamata majambazi hao wawili na ambao walitoroka.

Uvamizi huo unajiri mwezi mmoja tu baada ya mfanyibiashara mwingine wa Mpesa mjini humo kuuliwa kwa kupigwa risasi na majambazi.

KATIKA KAUNTI YA KISUMU: Nikuwa....

Shuguli za usafiri wa kawaida zilitatizika kwa muda kwenye barabara ya Mamboleo - Miwani, kaunti ya Kisumu baada ya wahudumu wa bodaboda eneo hilo kushiriki maandamano ili kulalamikia hali mbovu ya barabara sehemu hiyo.

"Hapa mamboleo tunaumia, vumbi inajaa kwa macho na madaktari wamegoma hawawezi kutuhudumia, tunauchungu kwa maana tunaenda katika hospitali ya kibinafsi ambayo ni mepa nyingi tunaomba Anyang'Nyong'o atusaidie," Alizungumza mwanabodaboda.

Kulingana na wahudumu hao walioishia kufunga barabara hiyo, wamelalamikia hatua ya barabara hiyo kuwa mbovu wakisema afya zao zimedorora kutokana na vumbi nyingi iinayoshuhudiwa.

"Barabara imejaa vumbi takataka zina pita hapa na lori hawataki kujua sisi ni akina nani wanapita hapa mbio hata hatuwezi fanya kazi nio maana tumefunga barabara," Alisema mwendeshaji mmoja wa pikipiki.

Wahudumu hao wamemtaka gavana wa kaunti ya Kisumu Prof. Peter Anyang' Nyong'o kuingilia kati kutatua changamoto hiyo na kutoa agizo la barabara hiyo kunyunyiziwa maji ili kupunguza vumbi.