Wauguzi wawili kupokea matibabu baada ya kushambuliwa na wagonjwa

mama Lucy hospital
mama Lucy hospital
Ni masaibu waliokumbana nayo wauguzi wa hospitali ya Mama Lucy, jumamosi usiku waliposhambuliwa na wagonjwa wawili na kuwaacha na majeraha.

Si kisa cha kwanza kutokea katika hospitali bali hicho ndicho kisa cha pili wauguzi kuvamiwa na wagonjwa, ina maana hawakuweka maanani kisa cha kwanza kutendeka?

Kulingana na polisi raia wawili waliweza kuwasili katika hospitali hiyo ya mama Lucy kisha wakawaambia wauguzi waweze kuwahudumia kwa haraka ilhali hawakuwa wamefuata utaratibu unaofaa.

Wauguzi hao waliweza kukataa madai ya raia hao na kusema kuwa wana wagonjwa wa dharura ambao walikuwa wanaenda kuwahudumia kwa haraka.

Kuvumba na kuvumbua wauguzi walijipata mahali pabaya, kwa maana wagonjwa hao waliweza kuwashambulia wauguzi kisha kuwaacha na majeraha, ambapo muuguzi mmoja aliweza kuumiwa mkono.

Watu wawili tayari wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho na wanatarajiwa kuwa mbele ya mahakama leo ilikueleza kwa kina kilichotendeka.

Ina maana kuwa wauguzi na madaktari hawana ulinzi wa kutosha katika hospitali nyingi? Wagonjwa hao hakuweza kuelewa kuwa wauguzi wengi wako kwenye mgomo na kisha kusubiri.

Polisi wanaendelea kumtafuta mmoja wa washambulizi kuhusiana na kisa hicho ambaye aliweza kutoroka baada ya kutenda kisa hicho.

Wauguzi hao walikuwa katika kazi yao kisa hicho kilichowakumba na kuacha mmoja wao akiwa amevunjika mkono.

"Wagonjwa hao waliingia hospitalini na kutaka kuhudumiwa kwa haraka kisha muuguzi mmoja akakataa na kusema kuwa ana wagonjwa wengine wa kuwahudumia kwa hivyo wasubiri,

"Ndipo waliweza kukasirika na kuwashambulia wauguzi hao,"Alieleza naibu mkuu wa Embakasi Kenneth Gitonga.

Wauguzi hao walisema kuwa mmoja wa wagonjwa alikuwa na kidonda katika shavu lake la  kushoto, alipomaliziwa kutibiwa huduma ya kwanza aliweza kuambiwa aweze kujisajili kirasmi kwenye hospitali hiyo kisha akakataa.

Kwa sasa polisi wamewekwa kulinda eneo hilo uchunguzi unapoendelea.