PATANISHO: Babangu alitutoroka tukiwa wadogo kwa miaka 11

patanish
patanish
Ruth alituma ujumbe akiomba asaidiwe kumuomba babake bwana Josphat Wambua, msamaha baada ya wawili hao kukosana sana.

"Babangu alituacha tukiwa class 7 na akaenda kazini, sasa akawacha kuja nyumbani na kwenda kabisa. Tukimpigia simu ilikuwa inachukuliwa na mama mwingine na huyo mama akatuambia tumsahau huyo ashakuwa mzee wake na tumsahau kabisa.

Mimi nilipomaliza darasa la nane mamangu hakuwa na karo na ilinibidi nirudie darasa la nane, baadaye nikapita mtihani nikapewa ufadhili shule ya Loreto.

Sasa ufadhili haukuwa wa fedha nyingi na nikimwambia babangu anasema niende niolewe au nifanye kazi za nyumbani kwani hawana haja nami.

Baada ya kumaliza chuo kikuu nikamwalika kuja katika sherehe za kufuzu lakini hakuja, ila tu marafiki zangu na mamangu. Sasa nikapata ufadhili wa kwenda kusomea Mexico na Germany lakini nikimwambia anisaidie na kitambulisho chake napata vitisho.

Nishapata Visa lakini siwezi pata passport bila kitambulisho cha babangu." Alieleza.

Ruth amezaliwa katika familia ya watoto watatu.

Alipopigiwa simu alisema kuwa Ruth pamoja na mama yake walitoka kwao na kutoroka.

"Unajua nilikuwa nafanya kazi mahali mbali kidogo, na kurudi nyumbani sikuwapata halafu waliambiwa kuwa nilipata mke mwingine nilipokuwa nafanya kazi." Alisema Mzee akiongeza kuwa aliyekuwa mkewe alipotoka nyumbani alienda na kuolewa tena.

Alisisitiza kuwa alijaribu kusuluhisha maneno kati yake na mamake Ruth lakini alikataa.