Shida zangu zinatokana na kusaidia watu - Bahati alizungumzia utata

Akihudhuria Malaika Tribute Awards Jumatano, msanii Bahati aliweza kuongea mwishowe na kuzungumzia utata ambao unamkumba kwa sasa.

Msanii ameweza kutuhumiwa kwa kumuitiapolisi  bibi ya msanii Seed Nimo Gachui, na kisha kukataa kulipa Mr Seed pesa zake.

Bahati alikataa kuguzia kisa cha msanii Mr Seed kutoka katika kampuni ya EMB, lakini katika mahojiano alisema,

"Shida yangu kubwa ambayo nimekuwa nayo kutoka Disemba ni kutokana na ukweli kuwa huwa nawasaidia watu,

"Lakini mwisho mwa siku utaweza kusaidia, kwa sababu baraka za mtu huwa zinatokana na kusaidia." Alisema.

Akiongeza alisema kuwa hajawahi kujibu mambo kama hayo, "mambo yangu mingi huwa tu inaendelea kama kawaida".

Aliendelea na kusema...

"Unavyo itwa na Mungu huwa unamgonja ili akupe maneno yanayofaa, unapoanza kuongea bila usaidizi wake ama mwongozo wake,

"Utashtukia tu umeharibu kila kitu na kuongea kando na ambacho ungefaa kuongea, mungu huwa anaongea kwa wakati wake, anaweza kawia lakini itakuja kupita." Alizungumza.

Alieleza kwanini hajawahi jibu madai hayo ambayo wasanii wengi wameweza kusema na pia mwingine kujitokeza na kusema kuwa amemdai Bahati.

"Biblia inasema katika kitabu cha James 1:9 Wapenzi ndugu zangu, kumbukeni haya, kila mtu anapaswa kuwa na haraka ya kusikiza, mpole kwa kukasirika na mpole pia kwa kuongea,

"Ndio maana huwa sikasiriki haraka." Bahati alieleza.

Aliweza kuongea na kupunguza sauti yake na kuuliza waandishi "kama singewahi kuwa simgefunga duka zenu?

Akiongeza.." Nyinyi watu mmeandika zaidi ya mada 19 kunihusu." Aliongeza Bahati.

Mke wa aliyekuwa maneja wake Mutua aliweza kuandika ujumbe mkali kwa Bahati akimuita atoke katika biashara yake sugu.

Ufuatao ni ujumbe ambao mwanamke huyo aliweza kuandika..