PATANISHO: Mila na desturi zetu hazituruhusu kubembeleza mwanamke!

Jamaa kwa jina Thuranira alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Kathure, akisema kuwa walikosana mwezi wa Disemba baada ya kumuumiza vibaya.

"Nilijawa na hasira na nikamtandika bibi yangu baada ya kumpiga mtoto wetu." Alisema Thuranira.

Niliingia kwa nyumba na mke wangu akaanza kusema kuwa nimetoka kwa wanawake wangu na akamzaba mtoto kofi. Baada ya kumpiga aliondoka na kwenda kwao." Aliongeza huku akisema aliwahi enda kwa baba mkwe kumjulisha kuwa yeye na mkewe hawako pamoja.

Aliongeza kuwa aliwahi mpigia mkewe simu lakini "Akijibu simu kwa maringo nakatiza mawasiliano." Huku akiwaacha watangazaji wakiwa na wingi wa kicheko.

Bwana Thuranira na Kathure wamekuwa kwa ndoa ya miaka tisa na wamejaliwa watoto wawili ambao aliwaendea nyumbani kwa mkewe.

Alipopigiwa simu bi Kathure alikiri kuwa apewe mda apumzike kwani amechoka na maneno ya mumewe.

"Kama umeamua kunipeleka Radio Jambo hiyo haina shida." Alisema Kathure.

Kile alinitendea sio vizuri kwani huwa na tabia ya kunipa na kunifanya nimwage damu. Hata kama nilipiga mtoto kwani sina amri ya kumpiga? Sitarudi kwake na ajipange na maisha." Aliongeza Kathure.

Kwa mila na desturi za kimeru hatuwezi bembeleza mwanamke! Alikiri Thuranira baada ya mkewe kukataa kurudi nyumbani.

Hata hivyo mkewe alifichua kuwa mumewe ana mwanamke ambaye amemfungulia akaunti na kumtumia fedha na mimi bado.

&feature=youtu.be