Mtoto wa miaka minane ajitia kitanzi huko Kakamega

Mtoto wa miaka minane amejitia kitanzi kwenye chumba cha bafu lao eneo la ikonyero viongani mwa mji wa Kakamega.

Familia ikiongozwa na mamake Lucy Makube imesema haina ufahamu wowote wa kilichopelekea kisa hicho.

Kwingineko

Askofu wa kanisa katoliki jimbo la kakamega Joseph Obanyi amepuuzilia mbali madai kuwa kanisa limenyamaza kuhusu swala la ufisadi nchini

Askofu Obanyi amesema vita dhidi ya ufisadi vimezungumziwa pakubwa na changamoto ni viongozi wanaohusika na ufiadi na amewataka wakristo kuwa msitari wa mbele kupigana vita hivyo.

Kwingineko

Baraza la magavana limeisuta serikali kuu kwa kukosa kutekeleza ushirikiano na serikali za kaunti kuendeleza maswala ya ufisadi.

Kwenye mazishi ya aliyekuwa meneja mkuu wa kampuni ya Nzoia Michael Kulundu aliyesemekana kutekwa nyara na kasha kufariki akipokea matibabu, mwenyekiti Wycliffe Oparanya amesema usalama ni jukumu kuu ambalo kaunti hazipaswi kuachwa nje.

Kwingineko

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Taita Taveta wameanza mchakato wa kuwarai wakaazi kutia sahini pendekezo la kaunti hiyo kulishtaki shirika la KWS kufuatia ugamvi wa mapato ya mbuga ya Tsavo.

Wanasema wanastahili kutengewa angalau asilimia 25% ya mapato yanayotokana na mbuga hiyo.