2 wapigwa risasi Mandera

Watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi walipokuwa wamelalakatika eneo la Forra karibu na Gar Shabba Mandera usiku.

Shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa nane usiku wa kumkia leo. Waliouawa ni mzee mmoja na mwanamume wa umri wa kadri.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi katika kaunti ya Mandera Steve Oloo alisema kwamba washambulizi hao waliwapiga risasi wawili hao wakiwa wamelala, amesema chifu wa eneo hilo aliitisha usaidizi kutoka kwa polisi. Waliouawa ni Abdul Jillo mwenye umri wa miaka 65 na Jillo Sora wa miaka 37.

Kamanda wa kaunti amekikashiru kitendo hicho na kutoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa kwa polisi ili wahusika wakamatwe.

Waliotekeleza mauaji hayo walitoroka punde tu baada ya mauaji hayo. Hakuna mifugo walioibwa wakati wa kisa hicho. Polisi bado hawabaini kiini cha mauaji hayo.

Kisa kama hicho kilifanyika Jumamosi iliyopita wakati mwanamume alipigwa risasai na kujeruhiwa vibaya.