PATANISHO: Kijana wangu atoe mbuzi au anipe elfu kumi

Stanley Muthomi aliomba apatanishwe na babake mzazi bwana Andrew, ambaye walikosana kupitia ugomvi kati yake na mkewe na hapo babake akadai kuwa amemkosea heshima.

Alisimulia,

Tulikosana na bibi yangu na baadaye alipoelekea kwao hapo ndipo mzazi wake alinipigia simu na kusema kuwa nisimfuate na hata huyo mtoto wetu sio sisi tumezaa ila ni yeye amezaa.

Hapo nikampigia babangu na kumueleza yaliyotokea na kwa hasira pia nikazungumza maneno na babangu hakunielewa na akasema kuwa sijamzaa na kuwa kamwe nisiseme kuwa mimi ni mwanawe.

Isitoshe babake Stanley alisema kuwa anafaa kwenda nyumbani kwao na achinje mbuzi ambayo italiwa na wazee wa njuri ncheke, shida kuu ni kuwa hana fedha kwa sasa.

"Huyo kijana alinikosea vibaya sana na nikamuambia chenye atafanya kwani mimi ni mzee wa Njuri Ncheke sio wa kukanyagwa ivo ivo, kwa hivyo lazima atoe mbuzi.

Sijakataa alichosema lakini hajatimiza tuliyozungumza kwani kunipeleka kwa redio haitamsaidia." Alisema bwana Stanley.

Stanley ambaye alipata ajali na kuumia miguu anasema hana kazi kwa sahii kwani alikuwa anafanya kazi ya bodaboda na kuwa sahii hawezi pata fedha za kununua mbuzi.

"Unajua huyo kijana angesema kuna kitu sijamfanyia ingekuwa afadhali, isitoshe mimi ndiye nimemnunulia bodaboda kwa hana heshima kabisa." Aliongeza mzee Andrew.

Alisisitiza kuwa hata mbuzi yenyewe sio ya elfu tano bali elfu kumi!