Kutana na balozi mpya ajaye wa Uingereza humu nchini

Mtaalam wa kupambana na ugaidi  Jane Mariott ndiye balozi ajaye wa Uingereza humu nchini  kuanzia septemba mwaka huu . Ataichukua nafasi ya Nic Hailey  ambaye amekuwa nchini tangu mwaka wa 2015 .  Mariott  mwenye umri wa miaka 43 atakuwa  mwanamke wa kwanza kuteuliwa balozi wa Uingereza humu nchini.

Bi.Mariott amewahi kuwa balozi wa Uingereza nchini Yemen   kati ya mwaka wa 2013-2015 na maajuzi amekuwa mkurugenzi wa  Kituo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi . Pia amewahi kuhudumu kama  mshauri wa Richard Holbrooke aliyekuwa mjumbe maalum wa uingereza katika mataifa ya Pakistan na Afganistan .

Katika ujumbe wake kwenye Twitter amesema amefurahia sana uteuzi wake kuja Kenya na atafanya kila juhudi kuboresha uhusiano kati ya Kenya na Uingereza .