PATANISHO: Siwezi mlaumu shetani kwa kuwa na mpango wa kando

Zablon na mkewe, Shomo, akisema kuwa alifumaniwa na mke mwingine na akakasirika na kupelekea wawili hao kutengana.
"Alipata message kwa simu mara tatu kutoka kwa wanawake watatu na hapo tukagombana na tukagawana mali yetu na kila mtu kwenda zake." Alisema Zablon.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka mitano na wamejaliwa mtoto mmoja wa miezi saba.

"Naweza sema ni majaribu hunifanya najipata kwa mambo haya, siwezi mlaumu shetani kwani sijawahi muona na sijui sura yake nitamlaumu aje?"

Alipopigiwa simu mkewe Zablon alisema kuwa hana shida ya kurudiana na mumewe lakini ana shida ya kuwa na mwanamke wa kando, na hataki kuwa mke wa pili.

Mara ya kwanza nilihamisha kila kitu na nikaenda kwetu na aliponiambia turudiane nikarudi na kila kitu. Round hii aliniambia kama anaenda atabeba kila kitu na akaenda na kuniacha bila chochote.

Nimeishi nikikuambia kama utawachana na huyo mwanamke basi nitarudi lakini mambo ya ku share siwezi kabisa. Ebu kumbuka miaka yote tumeishi nawe ni siku gani nimekuonesha madharau? 

Uliniambia huwezi wachana na huyo mwanamke kwa sababu ana mimba yako. Alisimulia bi Shomo.

Ili kumfurahisha na kumthibitishia bi Shomo, bwana Zablon alilishwa kiapo na bwana Ghost.

Bi Shomo alisema kuwa hana shida kurudiana na Zablon iwapo tu atawachana na mpango wa kando.