Lazima kuku mweusi achinjwe! Kabla ya Sharon na Melon kuishi pamoja .

   Wasichana pacha  ambao waliunganishwa baada ya miaka 19  wakiishi na familia mbili tofauti  lazima wafanyiwe tambiko  kabla ya kuishi pamoja kama familia moja . Mahojiano na wazee kutoka jamii ya waluhya   yameonyesha kwamba matambiko hayo ni ya kuzuia kurejelewa kwa tukio kama lililowasibu wasichana hao katika kizazi chao .

Matokeo ta DNA  yaliyotolewa siku ya jumamosi  yalionyesha kwamba  Melon Lutenyo na Sharon Matias ni madada wa damu moja .wawili hao walilelewa na mama tofauti hadi walipokutana kupitia  mitandao ya kijamii .Melon amelelewa na mamake mzazi  Rosemary Onyango ilhali Sharon amelelewa  na Angeline  Omina mtaani Kawangware hapa Nairobi  walipobadilishwa wakiwa katika shule ya chekechea .

‘Wazee lazima wamchinje kuku  mweusi ambaye hajataga  na kutayarisha dawa za miti shamba  ambazo zitanyunyuzwa karibu na lango kuu la boma lao ili kumaribisha binti yao ambaye hakuwa nao kabla ya mlo  wa familia nzima’,amesema  Ndeta  Chimasia  anayeisitiza kwamba lazima kuku huyo awe mweusi .