PATANISHO: Ndugu yangu ni mkali hata anaogopwa na chifu

patanisho
patanisho
Bwana George, 36, aliomba apatanishwe na nduguye bwana Victor, na hata aka katakata ng'ombe wa ndugu yake mkuu mwenye umri wa miaka 40.

Kulingana naye walisumbuana kwa ajili ya shamba licha yake kumsaidia na isitoshe ng'ombe wa nduguye alikula mimea yake. Anadai alimkata kata yule ng'ombe lakini hakumuua.

Wawili hao hawajakuwa wakizungumza na amekuwa akitishiwa kuwa atafute shamba mahala pengine.

"Ni George? Mwambie aje nyumbani hii mambo ya hewani mimi sitaki kuskia." Alisema Victor huku bwana George akisema kuwa anahofia atauliwa.

"Nilimuongelesha na ubaya wake anatuma text mimi namwambia aje nyumbani na sisi tuko wawili pekee nyumbani na sisi pekee ndio twaweza tengeneza boma."Aliongeza Victor akidai nduguye ni kichwa ngumu.

Upande wake George alisema kuwa nduguye ni mkali na kwa hilo hata chifu wa mtaa wao anamuogopa.

Nilikuwa na hasira naye na nimeshuka chini sana na nimekuwa nikimtafuta tuongee na amekuwa akinihepa, asitumie watu wengine waje waniongeleshe.

Alidhibitisha kuwa hatamdhuru wala kumfanyia lolote nduguye na kuwa anatumikia watu wengi.

Kwa upande wake bwana George alisisitiza kuwa ana uwoga baada ya kufukuzwa nyumbani na mkuki.