5 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Machakos-Wote

Watu watano walipoteza maisha Jumatano jioni baada ya matatu ya abiria 14 kuhusika katika ajali ya barabarani karibu na kituo cha kibiashara cha Muumandu kwenye barabara ya Machakos-Wote.

Watu wengine 13 wamelazwa katika Hospitali ya Machakos Level 5 wakiuguza majeraha mabaya.

Ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa gurudumu la matatu hiyo na kuipelekea kubingiria mara kadha katika kisa hicho cha mwendo wa saa moja unusu jioni.

Ajali hiyo ilithibitishwa na mkurugenzi wa huduma za dharura katika kaunti ya Machakos David Mwongela. Alisema kwamba matatu hiyo inamilikiwa na Maptra Sacco na mbali na kuendeshwa kwa kasi ya juu ilikuwa na abiria kupita kupita kiasi.

Alisema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ma kubingiria mara kadhaa na kuua watu watano papo hapo.

Majeruhi walikimbizwa hospitalini katika ambulansi ya kaunti ya Machakos na wengi wao wameimarika.

Alisema ajali hiyo ilisababishwa na uendeshaji mbovu wa gari na kukosa uajibikaji.

Miili yao inahifadhiwa katika Chumba cha wafu cha hospitali ya Machakos huku mabaki ya matatu hiyo yakipelekwa kwa kituo chas polisi cha Machakos.