Wamlambez! Tazama ujumbe wake Ghost Mulee kwa wanajambo

Leo ni Friday ama ukipenda, furahi day na mtangazaji Ghost yuko kwenye mood ya sherehe huku wikendi iking'oa nanga rasmi.

Katika kanda aliyochapisha katika mtandao wake wa Instagram, Mulee anaonekana akijiburudisha na kinywaji cha juisi ya miwa baada ya kutoka kazini.

Kwenye kanda hiyo, mtangazaji huyo wa Gidi na Ghost asubuhi, anawashauri mashabiki wake kutobugia pombe na kisha kuendesha magari.

Hata hivyo aliwakumbusha kuwa kama ni lazima wanywe na waendeshe magari basi wajaribu kunywa juisi ya miwa.

"Usione wivu ni ile tu nakunywa sugarcane juice ni Friday, na ndio mimi huwaambia kama unataka kunywa usinywe na uendeshe magari na kama unakunywa juisi ya miwa basi waweza endesha magari wakati wowote." Alisema Mulee kabla ya kuangua kicheko anachotambulika nacho.

Baadaye, Mulee alimalizia ujumbe wake kwa kuwatakia mashabiki wake wikendi njema akisema 'Wamlambez'.

Tazama kanda hiyo hapa.

https://www.instagram.com/p/Bzz6O13FY3x/