Chui apatikana kitandani baada ya mafuriko makali

chui
chui

Chui jike ambaye alitoroka mbuga ya wanyama ya India iliyokumbwa na mafuriko katika jimbo Assam alipatikana akiwa amejituliza kwenye kitanda cha mkazi mmoja ndani ya nyumba.

Inaaminiw akuwa alitoroka kutoka mbuga ya wanyama ya Kaziranga , ambako wanyama 92 wamekufa sihu za hivi karibuni kutokana na mafuriko makubwa.

Maafisa kutoka hifadhi ya wamnyamapori walilazimika kwenda kwenye nyumba hiyo, ili kuiondoa ndani ya chumba cha kulala.

Aliongozwa kuelekea kwenye eneo la msitu la mbuga.

Kwa mujibu wa shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini India (WTI), kwa mara ya kwanza chui huyo jike alionekana kwenye barabara kuu iliyopo karibu Alhamisi asubuhi, yapata kilomita 200 kutoka mbuga ya wanyama ya taifa.

Huenda alisumbuliwa na barabara yenye magari mengi na hivyo kuamua kutafuta maficho ndani ya nyumba ambayo , ilikuwa karibu na barabara kuui, alisema.

Mwenye nyumba kwa jina Rathin Barman, ambaye aliongoza shughuli ya kumuondosha chui huyo kwenye kitanda chake , amesema kuwa chui huyo aliingia nyumbani kwake ambayo iko karibu na duka majira ya saa moja ujunu asubuhi halafu akasinzia kwa siku nzima.

"Alikuwa amechoka sana na alikuwa na siku ya usingiizi mtamu ,"aliiambia BBC.

Mmiliki wa nyumba ,Motilal, ambaye anamiliki pia msururu wa maduka , pia alitoroka kwake na familia alipomuona chui akiingia ndani ya nyumba.

"Jambo zuri zaidi ni kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyetibua usinginzi wake kwa hiyo alilala fofofo . Katika eneo hili watu huwaheshimu sana wanyama ," Alisema Bwana Barman.

-BBC