PROOF:Niko tayari kwa uchunguzi wa DNA,asema ‘mke wa pili ‘ wa Ken Okoth

   Mpenzi wa kisiri wa aliyekuwa  mbunge wa Kibra Ken Okoth  Anne Thumbi amesema yuko tayari kwa uchunguzi wa DNA   ili kuthibitisha kwamba mtoto wake mvulana mwenye umri wa miaka mitano ni wa  marehemu mbunge huyo .Thumbi ameliambia gazeti la The Star   kwamba ingawaje hakuwa tayari kufichua uhusiano wake wa siri na Okoth ,yuko tayari kuthibitisha kwamba  mtoto huyo ni wa Okoth." Bado naomboleza ,sipo katika hali ya kuzungumzia suala hilo .Kama mnavyojua  suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama .Lakini niko tayari kwa vipimo vya DNA  iwapo watu wakiwemo familia ya Okoth  wana  shauku endapo mtoto huyo ni wake’ amesema  mwakilishi wadi huyo mteule . Alizungumza muda mfupi tu baada ya hakimu mkuu G.A Mmasi kutoa  agizo la kuwazuia mama ya Okoth na mkewe  Monica Okoth dhidi ya kumzika au kuuchoma mwili wa mbunge huyo kabla ya kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo .

“ Baada ya mtoto kuzaliwa ,marehemu  alikubali kwamba mtoto alikuwa wake na kuchukua majukumu ya uzazi  kwa kushughulikia maslahi yake na yangu alipokuwa hai’ Thumbi amesema .‘Okoth  alikuwa baba mzuri na kabla ya kifo chake alikuwa akitekeleza majukumu yake kama baba ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa mwanawe  ana nguo ,burudani na karo ya shule miongoni mwa gharama nyingine’  ameongeza Thumbi .  Mwakilishi huyo wa kaunti ameserma alikuwa akiwasiliana na Okoth mara kwa  mara alipokuwa akiugua  na nyakati za mwisho  za maisha yake . ‘Alitaka kwamba Mrithi wake wa pekee  aliyebeba jina lake atunzwe na kutambuliwa ili kuendeleza kizazi chake , jambo ambalo aliniambia na pia kuwafahamisha ‘watu wa   karibu wa familia yake’ Thumbi amesema .Thumbi  ameongeza kwamba mtoto huyo anafahamika sana na watu wa familia ya Okoth akiwemo nyanyake ambaye  amekutana na kutangamana naye kwa muda  tangu mjukuu wake alipozaliwa .

Kupitia wakili   Elkana Mogaka,   amesema mtoto huyo amenyimwa haki ya kuhusishwa katika maazishi ya babake na tamaduni zote zinazoambatana na shughuli hiyo . “ Mamake Okoth na mkewe kwa bahati mbaya wamemtenga Muthoni(Thumbi) katika mipango ya maazishi na wamefahamu tu kuhusu shughuli hizo kupitia magezetini  na vymbo vya habari’ Mogaka amesema . Pia amesema familia hiyo iliamua  kuuchoma mwili wa Okoth  ili kuharibu DNA  miongoni mwa sababu nyinyine kwa lengo la kuondoa kabisa uwezekano wa  kupatikana ushahidi kwamba Okoth ndiye baba ya mtoto huyo .

Mtoto huyo anatarajiwa kuripoti shuleni Septemba mosi ,ilhali hakuna mawasiliano yaliyotolewa kuhusu  karo yake ya shule .Mama mtoto anataka mahakama  kuiagiza familia ya Okoth kupitia mali ya mbunge huyo kulipa  kiasi  kikubwa  cha fedha kwa wakati mmoja  zitakazotumiwa kama karo ya shule ya mtoto huyo . Thumbi amemshtumu mkewe Okoth Monica  kwa kumbagua mtoto wake akisema kwamba  ameonyesha ishara za ubaguzi wa rangi  dhidi ya mtoto pekee ambaye ni mrithi halali wa marehemu .Mkewe Okoth Monica ni mzungu .