Dah! Mapokezi makubwa Kiambu. Sonko wa masonko amwaga pesa kibao

Kituo chako pendwa hii leo kimekita kambi katika mji mkuu wa kaunti ya Kiambu katika zoezi nzima la kuwatunuku mashabiki sugu zawadi mzomzo. Sonko wa masonko alitua mji huo saa tatu asubuhi na kuchana soko nzima kwa udi na uvumba kuwatafuta washindi wanaofahamu The Phrase That Pays ya kituo cha Redio Jambo.

Kupitia swali mboga sana la kuitambua “The Phrase That Pays”, msikilizaji huwa anatuzwa shilingi elfu moja.Kwa kutengeneza bango na kuandika Redio Jambo Ongea Usikike, mshindi hutuzwa elfu 5 pesa taslimu.

Tazama picha za washindi:

  

Mchakato na mpango mzima wa kuwatunuku wasikilizaji na mashabiki sugu kwa zawadi kemkem mwezi huu wa Julai na Agosti unaingia wiki ya 4 kwa sasa. Katika wiki ya kwanza iliyoanza tarehe 15 Julai, jiji la Nairobi lilipata nafasi kubwa ya kutembelewa na sonko wa masonko katika viunga tofauti tofauti za mji mkuu.

Ziara hii Inayoratibiwa kufanyika kwa mwezi mmoja ilianzia mitaa ya Kangemi,Kinoo,Uthiru na baadaye

barabara ya Jogoo miongoni mwa mitaa mingine katika jiji la Nairobi.

Juma lililopita, sonko huyu alizuru miji ya bonde la ufa kama Bomet, Kapsabet, Kipsitet na baadaye kuzamia Narok . Hii ni baada ya kuwatunuku mashabiki hela kibao katika miji mikubwa magharibi mwa Kenya.