Otile hakuninunulia gari! Jovial amwambia Massawe Jappan

Jovial mmoja wa wanamziki wakubwa waonaochipukia alihojiwa na mtangazaji wetu Massawe Jappani.

Mwanamziki huyo kwa jina Juliet Miriam Ayub alizaliwa mjini Mombasa na amekuwa akipanda kimziki kwa kasi.

Massawe alimuuliza kuhusu gari analodaiwa kunununuliwa na Otile na akakanusha madai hayo akisema kwamba sio ya ukweli.

Massawe pia alimuuliza Jovial ni lini aligundua kuwa na kipawa cha kuimba.

Alisema kwamba alianzia uimbaji wake katika kanisa la kiangiliakana huko Mombasa.

Alieleza kwamba wanamziki wa kike kutoka Kenya waliokatika mawazo yake ni Vivian na Nadia Mukami.

Mwanamziki huyo pia alimwabia Massawe kwamba yeye hutunza sana sauti yake kwa kunywa maji mengi yakiwa na ndimu na tangawizi.

Pia alisema anawaenzi sana wanamziki Diamond Platnumzi na Ali Kiba. Alisema Diamond anajua sana kujinadi.

TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO