Ilikuwaje; Pasta Ng'ang'a aeleza jinsi alivyojizolea wafuasi Kanisani mwake

Pastor Ng'ang'a amekuwa muhubiri mkubwa sana hapa nchini Kenya huku hivi karibuni akigonga vichwa vya habari kufuatia mzozo kanisani mwake. Ng'ang'a mwenye umri wa miaka 66  amekuwa mgeni wetu kwenye kipindi cha ilikuwaje na Massawe Japanni.

Ng'ang'a alianza kufanya kazi mwaka 1965 huku akilipwa mshahara wa shillingi sita na wazungu kwa kufanya kazi ya kuchunga kondoo. Hata hivyo, mambo yalianza kumgeuka mwaka wa 1972.

"Mwaka 1972, nilikuwa napigana na mtu mmoja nikiwa na umri wa miaka 18 na hivyo ndivyo masaibu yalinianza. Nilitiwa mbaroni na kupelekwa jela ambako niliishi miaka ishirini hadi mwaka wa 1992."

Akiwa gerezani, pasta anaeleza kuwa alipatana na muhubiri mmoja aliyemtabiria kuwa mwenyezi Mungu atambadilisha na kumpa neema maishani mwake. Alipoachiliwa, alianza na kazi ya mkokoteni. Mwaka wa 1995, pasta anaeleza kuwa wito wake Mungu ulimgusa. Wito wake Mungu na bidii ndizo chanzo cha wafuasi wake kuwa wengi.

"Nilifungua duka hapo Mombasa na kuanza kuuza maembe. Nilikuwa nahubiri kisha nakuja kufungua duka langu. Walimwengu sio wakuaminika na hivyo, wahubiri wa kanisa nililokuwa walinifukuza kwa madai ya kujifanya muhubiri huko nje kila wakati nikitoka kanisani."

Kulingana naye pasta Ng'ang'a, ukiwa na wito mwenyezi mungu hawezi kuacha uteseke hivyo lazima atakupa samaki kama alivyo wafanyia Petero walipoenda kuvua  samaki. Baada ya kufukuzwa, pasta alifanikiwa na kuanzisha kanisa lake.

Ng'ang'a anasema kuwa sio lazima usomee jambo fulani ili ufanikiwe.

"Nilifungua kanisa langu huko Mombasa na kuanza kuhubiri injili. Mwaka wa 2000, niliacha kanisa hilo lililokuwa na wafuasi zaidi ya 4500 huko mjini Mombasa na kuja haopa mjini Nairobi kufungua kanisa langu. Nilihamia Ng'ara na kufungua kanuisa langu kabla cijanunua mahali nimelijenga kanisa kuu kwa sasa."

Kando na sadaka, Pasta Nga'ng'a anasema kuwa yeye hujitegemea kwani yeye ni mkulima mkubwa sana pamoja na mfanya biashara.

"Mimi ni mkulima na mwaka uliopita nilikuwa na gunia mia tano za mahindi. Kabla nihame Mombasa nilikuwa na nduka kubwa lilokuwa linaniletea pesa.

Pasta Ng'ang'a amekubwa na kashfa nyingi hivi karibuni ila amejitokeza na kusema kuwa hizo zote ni porojo.

"Mimi sijawahi kumchapa mke wangu na pia ijulikane kwamba ndani ya ndoa lazima kuwa na mizozo midogo kabla ndoa hio haijakomaa. Pia, mimi sijawahi kunywa pombe kama ilivyokuwa inadaiwa wakai wa ajali iliyotokea mjini Naivasha. Niliitana mkutano na wakati watu walikuja mimi sikujua ni gari li[pi ila nilisikia baadaye kuwa kuna gari lilosababisha ajali na kuyapoteza maisha ya mkenya mmoja."

Pasta Ng'ang'a ambaye hivi juzi aliwakashifu makasisi kanisani mwake amesema kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya mkewe.

"Mkewe wangu ni mdogo kiumri hivyo hawakuwa wanamheshimu kila wakati akiitana mkutano jambo lilonikasirisha sana kwani natumai kuwa atanichunga siku zangu za uzeeni. Kama vile tulikuwa tunamtii baba tukiwa wadogo, namimi kwa sasa ndiye baba kanisani hapo na hivyo nikikohoa lazima mtu aitike!"

Kwa sasa Pasta Ng'ang'a anapania kuendeleza injili yake hadi ulimwenguni kote na hasa kupitia kituo chake cha televisheni.