Wakala wa sensa ahusika densi na watoto wadogo. Video yavuja na kusambaa Twitter

unnamed__1567416024_54678
unnamed__1567416024_54678
Wakala wa zoezi la sensa lililokamilika jumamosi ametamba katika mtandao wa Twitter baada ya kipande cha video kusambaa. Katika video hii inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, wakala huyu anapiga densi hatari na watoto wa umri mdogo wakimshangilia kwa mbwembwe za  "Mtu wa census".

Soma mengine hapa:

Collins Kiprono, alikuwa katika pilka za kuwahesabu watu katika kituo cha kurekebisha tabia cha Kericho alipohusika katika kitendo hiki kinachovuta hisia za wengi katika mitandao ya kijamii.

Mara ghafla Hashtegi ya  #MtuWaCensus ikaanza kutamba kama moto jangwani wikendi nzima. Shirika linalowajibika katika zoezi hilo Kenya National Bureau of Statistics (KNBS) limechapisha video hiyo na kumshukuru Collins kwa utendakazi mwema.

Soma mengine hapa:

https://twitter.com/KNBStats/status/1167808802244222977