Babake Diamond asimulia A-Z kilichomfanya Harmonize kutoka usafini WCB. Amtuliza Mondi kwa pigo hilo

DIAMOND_FATHER__1560931468_42764
DIAMOND_FATHER__1560931468_42764
Baada ya mzee wa Mondi kukosolewa na mashabiki wake baada ya kuchapisha video ya Harmonize katika mtandao wake wa insta. Sasa Baba Dangote ametokea na mapya na kufunguka A-Z kilichosukumia Harmonize atangaze kuitema lebo ya WCB. Baba Diamond amesema kuwa kutoka kwa staa huyu kutoka lebo sio kitu cha kushtukiza kwani dalili zilikuwepo.

Mzee Abdul anahoji kuwa dalili za Harmonize kuwa ana uwezo wa kufanya na kusimamia fiesta zake nje ya chi ni ishara kuwa mwana kashakua na kwa hivo kutoka kwake ni kwema kwa maslahi yake. Anadokeza kuwa labda dogo kapewa ushawishi na marafiki wake ili kufanya uamuzi huo.

Soma hadithi hii:

" Kwanza Naseeb alimuangaikia sana. Kamtufuta kampa sapoti kubwa kamtoa kimuziki," Mzee Abdul.

"Harmonize sio mtoto. Ukiona mtu anatoka kashakomaa tayari."

Soma hadithi hii:

Abdul amesema kuwa simu yake ina nyimbo kibao za WCB na ni shabiki mkubwa sana wa Harmonize.

"Chibu kama Chibu ni mwanangu. Simba tulia bado hujapoteza. Kaa tulia omngeza utapata mwingine zaidi ya huyo. Mwingine alitoka na kama wewe tulia komaa." Alimtuliza Diamond Platnumz.