Jamaa ashtakiwa kwa kuiba furushi tatu za karatasi ya tishu

tishu
tishu
Wiki iliyopita, Jamaa mmoja alishtakiwa kwa kuiba furushi tatu za karatasi ya tishu (tissue paper) katika chuo kikuu cha Strathmore.

Jamaa huyo kwa jina Benard Kibet alishtakiwa kwa kuiba furushi hizo zenye dhamani ya shilingi 300 ambazo ni mali ya Strathmore.

Kibet alishikwa baada ya Strathmore kupitia mkuu wa usalama Christian Angwenyi kupiga ripoti kwa kituo cha polisi. Kibet anashtakiwa kwa kujiwekea bidhaa ambazo vimeibiwa kwa manufaa yake mwenyewe.

Huku akiwa mbele ya hakimu mkuu Joyce Gandani, Kibet alikubali kuwa alitekeleza makosa yale. Akijitetea, alisema hakujua ilikuwa makosa kuchukua karatasi hizo za tishu.

Alipigwa faini ya shilingi 5000 ama kutumikia kifungo cha mwezi mmoja korokoroni.