Hata kanisa halikuweza kuniondolea uraibu wa Punyeto!

Katika kipindi cha Bustani la Massawe, binti mmoja alifungua roho na kusimulia vile ambavyo uraibu wake wa punyeto ulianza.

Amini usiamini, binti huyu alikuwa anajiburisha hata akiwa kanisani kwani hangeweza kuzuia hisia zake.

''Hata nikiwa kanisani ati pastor anahubiri huko mbele mimi niko tu hapa biashara''

Mrembo huyo kwa jina, Nashami Wangara, alianza tabia hii baada ya kupitia mengi na wanume aliokuwa nao katika uhusiano. Alieleza kwamba, alipokuwa katika  shule  ya upili, alikuwa binti mzuri sana.

Alitilia maanani masomo yake na kutia bidii ili afaulu masomoni. Hivyo basi, baada ya kumaliza shule ya upili, aliona kwamba ametimia umri wa  'kula maisha' na kufanya yote ambayo hakuwa anafanya akiwa shule ya upili.

Binti huyu alianza uhusiano na mwanamume aliyemzidi umri kwa miaka mitano,  akiwa na umri wa miaka kumi na saba pekee.

Licha ya kuwa bado na umri mdogo mara kwa mara alifanya yote aliyoambiwa na mpenziwe. Hata hivyo, baada ya miaka miwili, binti huyu alikosana na mpenzi wake na akapata mwingine na wengine waliomuumiza moyo na hapo ndipo akaamua kujitimizia mahitaji ya kimwili mwenyewe kwake alihisi kwamba raha ni kujipa mwenyewe.

"Nilichoka na wanaume na nikasema heee! Naeza jifurahisha pia, si lazima nifurahishwe na mwanamume.''

Uraibu wake ulipanda na kila siku alikuwa anajizuzua mwenyewe mara mbili.

"Nilikuwa najisatisfy kila siku, times 2 kama dawa unless otherwise mchana ndio nitama...tena'' alisema.

Hata hivyo, mwaka wa  2009, Wangara aliacha kabisa tabia hii baada  ya kusaidiwa na rafiki yake wa dhati kuacha  tabia hii.

''It got to a point I felt that I needed to change, na ndio nikatafuta mtu mwenye hawezi nikashifu and for 6 months, huyu rafiki alitembea na mimi na hata kama siku nyingine ningerudia tabia yangu, bado angeni encourage na kuniambia kuwa, anafocus on the good and the fact that I am improving.''Wangara alisema.

Zaidi ya hayo, Wangara alisema kuwa, ilimbidi abadili mienendo na kuangazia mambo ya maana kama vile kusoma vitabu na ndipo akafaulu. Hivyo basi, wakati ambao alikuwa anafanya punyeto aliutumia kusoma vitabu.

Mwisho, aliwapa wosia waraibu wa punyeto na kuwaambia kuwa endapo wanataka kubadili mienendo, wanafaa kuangazia masuala yenye manufaa.