William Ruto amjibu Waiguru. Tamko la Waiguru halikumpendeza

BILL
BILL
Siasa za ni nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta zinashadidi na kurindima kama moto jangwani licha ya Kenyatta kuwaonya wanaofanya siasa wakome.

Hali hii imekigawanya chama tawala katika tanzu la Kieleweke na tanzu lingine la TangaTanga.

Kieleweke linaaminika kuwa tawi linalounga mkataba wa Handshake kati ya Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga.

Soma hadithi nyingine:

TangaTanga nalo ni tawi la chama tawala linalofanya kila juhudi kuona kwamba Ruto ameuchukua usukani wa urais.

Siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa wanajua kuucheza.

Nikueleze kwamba matakwa ya wanasiasa huwavuta pamoja. Usishangae kuona wanasiasa katika urafiki wa kisiasa wakitengana na kila mmoja kuchukua njia tofauti.

Wakati kambi hizi mbili zinavutana, nguzo kuu na ambalo litatikisa wingu la maamuzi ni jinsi wapiga kura wa mlima Kenya wataamua.

Ikumbukwe kwamba jamii ya Kikuyu ina idadi kubwa ya wapiga kura nchini.

Tunasubiri kuona iwapo jamii ya kikuyu itateuwa mgombeaji wa urais atayempa tumbojoto na wasiwasi William Samoei Ruto.

Soma hadithi nyingine:

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru mapema wiki hii amenukuliwa katika vyombo vya habari akisisitiza kwamba jamii ya Kikuyu haiko tayari kumchagua tena rais mkikuyu.

Kauli hii ya Waiguru haikumfurahisha Ruto na akaamua kumjibu kupitia mtandao wa Twitter.

"Tulimuunga mkono na kumpigia kura Uhuru akamrithi Kibaki kwa ni misingi ya uchapakazi wala sio ukabila. Yeye sio kiongozi wa jamii yoyote ila ni kiongozi wa Jubilee..."

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1172095736718209026

Urafiki wa kisiasa kati ya Waiguru na Ruto unaonekana kuota mbawa. Sio kama zamani.