PATANISHO: Hata kura walirudia Gidi, tafadhali mjaribu mke wangu tena

Aliyeomba apatanishwe siku ya leo ni bwana Andrew akisema kuwa walikosana na mkewe bi Linet.
"Ile kitu ilitokea tulikosana wikimbili zilizopita na makosa ya kwanza nikitoka kazini nilikuwa napata amekunja sura na nashangaa nini mbaya. La pili nikamwambia aniimbie wimbo wa happy birthday na alipouliza tarehe na mwezi nikamwambia, hapo akaniambia hakuna aliyezaliwa hiyo siku." Bwana Andrew alisema.

Alisema alimpigia mamake na kumjulisha kilichotendeka. Hata hivyo siku moja alipakiwa chakula na akakipiga teke akitaka kujua chanzo cha mkewe kununa. Tendo hilo halikusaidia kwani mkewe alikasirika na kutoka na kwenda kwao.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wana mtoto ambaye aliondoka naye.

Bwana Andrew alibidi amtumia mkewe ujumbe kupitia radio baada ya simu yake kuzimwa.

Alisema,

"Linet kama unaniskiza tafadhali mtu hukosea na naomba unisamehe na ile kichwa ngumu unayo tafadhali rudi ubadilishe, tafadhali skiza bwana Gidi na urudi tulee mtoto wetu kwa sababu nahuzunika siendi kazi.

Sasa napitia mengi tafadhali rudi kama unaniskiza fungua simu."