Deejay asimulia alivyokatwa mkono na adui. Haki yake anaisubiri mpaka leo

41bf883c_153f_4f7f_9f85_e2dc50cfc4bd__1568727508_12945
41bf883c_153f_4f7f_9f85_e2dc50cfc4bd__1568727508_12945
Eric Kioko amesimulia jinsi alivyojipata katika mchafuko wa siasa mwaka wa 2008.

Jamaa ambaye ana uraibu wa Deejay alikuwa katika kipindi cha Bustani la Massawe na kusimulia haya.

Soma hadithi nyingine;

Eric anasema kwamba alikuwa Kisumu na uoga ulimvaa zaidi akiwaza kuwa huenda mzazi wake akawa katika hali sio nzuri.

"Nilikuwa kazi Kisumu. Mwaka wa 2008 nikafika Nairobi. Nilikuja kupotezea mkono mtaa wangu Mathare...ilikuwa ni usiku saa tatu mtu ninayefahamu akanikata mkono."

Eric ambaye anafahamika kama Deejay Talanta anasema kuwa alikatwa panga la kichwani na mkono wake.

"Nikasikia kitu imeanguka. Nikaona mkono una-move. Nikabebwa na soldier wa Airforce akanipeleka Kenyatta Hospital."

Soma hadithi nyingine;

Eric amesema kuwa hangeinama kuchukua mkono wake. Baada ya hapo akachukuliwa Hospitali ya Kenyatta.

Hadi leo Deejay huyu hajawafahamu mahasimu waliomkata mkono,

"Mungu anawajua.Ni kati ya mkaazi wa eneo hilo la Bondeni."

Katika mahakama nchini, sheria inajikokota sana na bado hajapata haki.

Soma hadithi nyingine;

Eric aliwahi kushiriki katika wizi kwa kipindi cha miaka 5 bila kupatikana na baadaye akaja kubadilika. Anasema kuwa mamake alikuwa anafahamu kuwa alikuwa akiiba mali ya watu.

"Nilikuwa naingia nyumba ya mtu naiba na kutoroka. Kukatwa mkono kulinibadilisha. Wengi tulikuwa tunaiba na wao ni marehemu."

Deejay huyu sasa anawaomba vijana wakome tabia za wizi na kumakinika katika maswala yanayojenga.

"Vijana waache kukaa idle. Hii ni njia moja ya kushawishika kuingia katika ualifu."