Mwanaume, 52 ahukumiwa kifungu cha maisha kwa kumbaka mtoto

Mwaname mmoja mweye umri wa miaka 52, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya Busia kwa kosa la kumbaka mtoto msichana wa umri wa miaka miwili.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Busia, Samson Temu alimpata mwanaume huyo kwa jina Habert Ateri Wasike na kosa la kumnajisi na kumficha mtoto huyo msituni, usiku wa tarehe 8/1/2018 mjini Malaba kaunti ndogo ya Teso kaskazini kaunti ya Busia.

Katika uamuzi wake, hakimu alielezea kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Mamake mtoto huyo amepongeza uamuzi huo akisema umempa utulivu moyoni baada ya kutafuta haki kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwingineko, Washikadau katika sekta ya afya Kaunti ndogo ya Webuye Magharibi wameafikia uamuzi wa kushirikiana katika utoaji huduma bora za afya, ushirikiano ambao utawawezesha kuwafikia wagonjwa wengi katika Hospitali ya Webuye.

Kwa mujibu wa Alfred Nyongesa, Afisa Mkuu wa afya Kaunti ndogo ya Webuye Magharibi Pamoja na Daktari msimamizi eneo hilo Florence Wabomba, kumekuwapo na maafisa wengi wanaotekeleza jukumu moja, hali inayostahili  kudhibitiwa.

Taarifa ya Leonard Acharry