Hali ilivyo Bahari Hindi, Bassen aeleza kuwa alivyodhania sivyo

wbanfynep9x5de4efu5d964c1f25cf2
wbanfynep9x5de4efu5d964c1f25cf2
Mpiga mbizi mswidi, Bassen ameambulia patupu katika juhudi za kuokoa maisha ya Mariam na mtoto wake Mutheu.

Imani ya ndugu zake Mariam kwa mswidi huyu ilikuwa ya juu sana.

Walisema moyoni kuwa Bassen atakuwa mwokozi aliyetumwa na Mungu kutegua kitendawil hicho.

Soma hadithi nyingine;

 Tofauti na taarifa za awali kuwa Bassen alikuwa na uwezo wa kujua ilipo gari na miili ya Mariam na mtoto wake, mswidi huyu alisema kuwa sio jambo rahisi kabisa.

Hii ni siku ya sita tangu gari ya mama na mtoto wake kutumbukia Bahari Hindi.

Ndoto ya kuwapata sasa inaonekana kuzima baada ya mpiga mbizi huyu kushindwa.

Soma hadithi nyingine;

"Nimegundua kuwa hali ilivyo hapa sio vile nilikuwa nakusudia..." Bassen alihadithia wanahabari.

Alikuwa na msemaji wa serikali Col Cyrus Oguna, familia Kighenda, 35, na vikosi vingine vya wanamaji wanaosaidia katika  juhudi za uokozi.

“Kufikia sasa, hatujaweza kufaulu," Msemaji wa serikali.

“Tutatumia roboti katika zoezi la kutafuta na kukusanya data," Alisema Oguna.

Soma hadithi nyingine;

 “Maji yana kina kirefu zaidi na kuna dhoruba kali ya maji ya Bahari Hindi. Hii inafanya mazingira tata ya kuipata gari," Alisema Bassen

"Halitakuwa jambo rahisi. Hiyo nina uhakika.' Bassen.

“Tutarejea Jumamosi (Leo) ili tuzidi kutafuta suluhu...Naomba tuwe na imani kuwa kesho itakuwa siku njema." Alisema Oguna.