Patanisho: ''Alinitusi kwa sababu mama yangu ni mgonjwa''

IMG_9832 (1)
IMG_9832 (1)
Katika kitengo chetu cha Patanisho, bwana mmoja jina lake Hussein alituma ujumbe na kusema kuwa, wamekorofishana na mke wake kwa sababu  anashuku ana mke mwigine.

Hata hivyo, binti huyu, Mama Aisha alipopigiwa simu alisema kuwa, mume alitoka kwake na kuhama kwa sababu mume wake alimtusi vibaya sana.

Vileile, Mama Aisha alifunguka na kusema kuwa alitoka kwake na kwenda kwao kwa sababu mama yake ni mgonjwa.

''Mimi niko kwetu kwa sababu mama yangu ni mgonjwa.''Mama Aisha alisema.

Licha ya hayo, wapenzi hawa, bwana Hussein na Mama Aisha walikubaliana na kuambiana maneno matamu baada ya baba Aisha kumwomba mke wake msamaha.