PATANISHO: Utakula sumu ukiendelea kunisumbua!

gidi na ghost asubuhi
gidi na ghost asubuhi
Alex alituma ujumbe akiomba apatanishwe na dadake bi Rose ambaye walikosana pindi tu alipomwambia aende akaolewe baada ya kupata watoto 5 nyumbani kwao.

Kulingana na Alex, dadake alimtishia kuwa atamuekea sumu kwa chakula.

Alex alisimulia,

Tulikosana kwa sababu dadangu alikuwa anajifungua kila mara na kila mtoto ana baba tofauti. Siku moja nikitoka Nairobi niliambiwa kuwa alikuwa anasumbua mama. Nikamwambia atafute mwanaume mmoja Kati ya wale waliomzalisha aishi naye.

Ubaya huwa haskii, ana Kiburi kwani akipachikwa mimba yeye huishi na yule jamaa na pindi tu anapojifungua, anaondoka. Wale baba wa watoto wanatuma fedha za watoto miezi mitatu pekee kisha wanaacha.

Alex anasema kuwa licha ya hayo, watoto wake wote wanalelewa na mamake mzazi Kule mashinani. Aliongeza kuwa wawili hao hawajazungumza kwa mda sasa na anashuku kuwa dadake ana nia ya kumuekea sumu kwa chakula.

Bi Rose alipopigiwa simu alimwambia Alex awachane naye kwani mzigo wake haufai kumhusu huku akimkumbusha kuwa yeye ni mtoto mdogo.

"Nikafariki leo hao watoto ni wewe utawasaidia kwani wewe ndio baba yao, ukizidi kunifuata sumu utakula." Alisema Rose.

Alex alichukua fursa ile kujieleza na kumsaidia dadake kuelewa shida yake ipo wapi.

Rose alijibu,

Hapo sasa umeongea na ule wakati ulikuja nyumbani ulileta vita. Huyo kijana mkubwa ni wa rafiki yako George. Kelvin naye kwao ni malaba, babake ni Ouma.

Purity kwao ni Bungoma babake ni Wanjala. Hao wengine wachana nao kwani babayao alipata ajali na akafariki."

Rose anasema hataki kuolewa Kwani ndoa yake ya mwisho aliteswa na ilibidi atoroke na hataki kurudia yale.

Wawili hao walisamheana na kuapa kuishi kwa amani huku Rose akiongeza kuwa hana nia ya kuongeza mtoto mwingine.