Ilikuaje:Ya Mungu ni Mengi!Mwanamke aliyepoteza maisha ya watoto nane ajieleza

IMG_9774
IMG_9774
Susan Wanjiru Ndung'u aliyekuwa mgeni wa kitengo cha Ilikuaje na Bi Massawe Japanni,alifunguka mwanzo mwisho na kueleza yaliyompata kila wakati alipojaribu kujifungua mtoto.

Bi huyu ambaye ni mama,mhubiri na hata mwanasayansi alisema kuwa,maisha hayo yalikuwa magumu  na alikuwa mwanamke mwenye huzuni sana.

Susan alisema kuwa alizaliwa na shida ya jeni (genes) na alipokuwa tayari kuwa mama ndipo akagundua ana shida ile baada ya kuwa na shida ya kutoweza kubeba ujauzito kwa miezi inayotakikana.

Amini usiamini,Susan alipoteza watoto saba kwa sababu ya kuharibikiwa na utumbo (Miscarriage) na wengine wawili wakazaliwa na kufariki.

Vilevile,binti huyu alisema kuwa hakupoteza matumaini ya kupata mtoto hata baada ya kupatwa na matatizo mengi ya ujiauzito kwa sababu alikuzwa katika familia ya kikristu ambapo mama yao aliwafunza kutokata tamaa maishani.

''Sikuwa nakufa moyo kwa sababu mama yangu alikuwa ametufunza tusiwe watu wa kukata tamaa kwani hata Ayubu alijaribiwa na hakukata tamaa.''Susan alisema.

Licha ya hayo,mhubiri huyu alisema kuwa, mume wake alijitolea mzima mzima kumsaidia na kumuunga mkono kwani hata kuna wakati ambao hakuwa anajiweza kabisa na bado mume wake alizidi kumpa msaada wowote ule alihitaji.

Aisee!Ni wazi kabisa kuwa Mungu hamuachi mja wake kwani baada ya kutibiwa ugonjwa huo binti huyu aliweza kujifungua watoto na kwa sasa ana mapacha na mtoto mmoja ambao wote wamekuwa wakubwa.

Mwisho kabisa,alizidi kuwaambia kina mama ambao wanapitia changamoto hili la kutopata watoto wasife moyo,waende hospitalini na  pia waombe Mungu na mambo yatakuwa shwari.