(+ Video) Mahangaiko ya Harmonize, Je lebo ya WCB inamnyanyasa ?

images (1)
images (1)
Harmonize amesimulia mahangaiko anayopitia baada ya kutangaza kuitema lebo kubwa Afrika Mashariki y WCB.

Katika mahojiano na Clouds, staa huyu amesimulia jinsi amelazimika kuuza nyumba zake kulipa Milioni 22.5 anazodaiwa na lebo ya Wasafi.

Uongozi wa WCB sasa unamtaka alipe hela iliyotumika kurekodi muziki wake na zaidi ya hapo kununua hatimiliki za jina la Harmonize.

https://www.instagram.com/p/B4CBTWQHrw3/

Ikumbukwe kwamba staa huyu anayetamba na mkwaju wa UNO hakuwa na jina hilo alipoingia Usafini (WCB)

Jina la Harmonize , Harmonize mwenyewe ni mali ya WCB kulingana na meneja wa Diamond Sallam SK.\

Kufikia sasa Konde Boy ameuza nyumba zake mbili katika juhudi za kumaliza mkataba wake freshi bila matatizo.

"Nimelipa kiasi lakini mpaka hivi sasa bado nadaiwa na sijamalizia kulipa ila bado kiasi kidogo sana cha kumalizia hela hiyo," Harmonize alidokeza.

Sikuwa na hela, kwa hivyo nikauza baadhi ya ninavyomiliki. Kuna sehemu nilikuwa najenga nyumba zangu 3, nililazimika kuuza. Nilifanya hivo kwa sababu pesa sio kitu. Nishawatumia mpunga kiasi fulani na salio ni ndogo..." Alisema Konde Boy

Ila je? Kuna uwezekano wowote lebo hii ikawa inamnyanyasa Konde Boy.

Msanii Rich Mavoko alipitia njia sawa na Harmonize.

Je, hela wanayodai wasanii hawa inaweza ikaathiri muziki wao wa njia moja ama nyingine?