Mkewe Peter Ndegwa amsifia, achapisha ujumbe wa kumpongeza

unnamed__1___1571986717_73149
unnamed__1___1571986717_73149
Mkewe Peter Ndegwa amemtumia mmewe ujumbe wa kumpongeza muda mchache baada ya kutangazwa mrithi wa Bob Collymore.

"Mpenzi wangu, hakika ni ukweli unavyosema kuwa hakuna njia fupi ya ufanisi katika maisha..." Alisema Jemima Ndegwa.

"Nimeshuhudia jinsi unavyotenga wakati wako kuwahudumia wengi pamoja na juhudi za kufika mbali..." alichapisha Jemima.

Peter ndiye Mkenya wa kwanza kuteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom .

Taarifa hizi zilitolewa na bodi kuu ya Safaricom jana Alhamisi.

Kwa mujibu wa bodi hii, Ndegwa ataanza kazi Mosi ya Aprili 2020.

Ndegwa alikuwa akihudumu katika kampuni ya Diageo iliyopo bara Ulaya.
Mwenyekiti katika kampuni ya Safaricom Nicholas Ng’ang’a alisema kuwa Ndegwa ana uzoefu mwingi katika usimamizi, mikakati ya kibiashara, na uendeshaji wa fedha kwani amefanya kazi hilo kwa muda wa miaka 25 katika majukumu mbalimbali ndani ya sekta ya huduma za kifedha.

Ndegwa atachukua nafasi ya Michael Joseph ambaye alihudumu kama afisa mkuu baada ya kufariki kwa Bob Collymore.

Collymore aliaga dunia mnamo juni mwaka huu baada ya pigano kali na ugonjwa wa saratani.

Taarifa kutoka kampuni hiyo ya mawasiliano ina matumaini kuwa Ndegwa atachangia pakubwa kubadilisha maisha katika jamii.

Safaricom inamilikiwa na Vodacom ya Afrika Kusini kwa asilimia 35%, serikali ya Kenya ina hisa asilimia 35%, asilimia 25% inauzwa katika soko la usalama la Nairobi, huku Vodafone group ina hisa ya asilimia 5%.

Safaricom inadhibiti takriban asilima 62% ya soko ya rununu ya Kenya.