'Nilinyang'anywa mtoto akapelekwa kwa mpango wa kando,' - Rozie

Yaweza kuwa mwongo mmoja tangia mwanadada kwa jina Rozie, kutendewa kitendo cha kuvunja moyo na aliyekuwa mumewe lakini bado kidonda hicho hakijapona moyoni.

Akielezea mtangazaji Massawe Japanni kwenye kitengo cha Bustani la Massawe, Rozie alifichua jinsi alipitia makuu mikononi mwa mumewe. Alieleza kuwa alikuwa anapigwa na kuteswa mara kwa mara.

Hakueleza chanzo au kilichopelekea mateso hayo.

Basi siku moja vita hivyo vilizidi na alipogundua kuwa mumewe alikuwa na nia ya kumuumiza, alitimua mbio ili kuokoa maisha yake huku akimuacha mwanawe nyuma.

Alisema kuwa mumewe alimchukua mwana yule aliyekuwa chini ya miezi sita na kumpeleka kwa mpango wake wa kando.

Rozie aliongeza kuwa mwanawe aligonjeka akiwa mikononi mwa yule mwanadada na hapo ndipo waliamua kumrudisha nyumbani. Miaka kumi baadaye, alipona ila bado hajamsamehe mumewe.

Soma usimulizi wake,

Nilitolewa mtoto kwa matiti na bwana na akapelekwa kwa mpango wa kando.

Nilipigwa na ile kukimbia niokoe maisha yangu akachukua mtoto akapeleka. Kupigia msichana simu akasema yeye ameambiwa aje akae na mtoto, nikamwambia mtoto wangu hutakaa naye.

Sasa mtoto wangu alifika huko akawa mgonjwa kwani alikuwa mdogo sana chini ya miezi misita. Alipokuwa mgonjwa ndio waliamua kunirudishia.

Mtoto alipona na imekuwa miaka kumi na bado kisa hicho kinaniuma mpaka wa leo. Ni ngumu lakini siwezi sahau.

&feature=youtu.be