Daah! Waume wa kanisani pia? Mwanamke auawa na mumewe

woman-killed
woman-killed

Inasemekana kuwa Jamaa mmoja kutoka nchi ya Ghana na mhudumu katika kanisa la Assembly of God, alimuua mke wake mwenyewe.

  

Mshukiwa, bwana Prince Korley Commodore mwenye umri wa miaka 48 alikuwa ameoana na mkewe bi Dorcas Anafi Commodore mwenye umri wa miaka 37 miaka 9 iliyopita.

Watoto wao, mabinti wawili wenye umri wa miaka mitano na mwingine miaka nane walikuwa kwenye chumba chao wakati ambao kisa hiki kilikuwa kinafanyika.
Mtoto mmoja alikuwa analia kwa sauti akisema,
''Baba unamuua mama?''
Mshukiwa huyu alikamatwa na maafisa wa Dansoman baada ya mauaji hayo. Baada ya uchunguzi maafisa walisema walipata kisu ambayo ilitumika kutoa maisha ya mama huyu.

Mwanamke ambaye alijitambulisha kama Bi Shirley Tackie, jirani alisema kuwa marehemu Dorcas na mume wake Prince Korley walikuwa na maisha mazuri sana bila mvurugano wala vita.

Zaidi ya hayo, binti huyu alisema kuwa kutokana na vile ambavyo anamjua Bwana Commodore hakuna mtu ambaye angeweza kufikiri kuwa bwana huyu anaweza kufanya kitendo kama kilecha kinyama.

''Tumewaona wawili hawa wakienda kanisani kila jumapili na kurudi nyumbani na furaha kila wakati.'' Shirley alisema.

Vilevile, mwanamke huyu alisema kuwa wawili hawa walikuwa wanahudhuria sherehe zozote au mikutano yoyote kanisani pamoja kila mara.

Ni dhahiri kuwa, wengi hawaamini kitendo hiki kwani si kawaida kwa binadamu haswa wanaomjua mungu kufanya kitendo kama hiki.

Mungu ailaze roho ya Bi Dorcas Anafi mahali pema peponi.