Utacheka ufe! Tazama jinsi wapigaji kura walivyojitokeza Kibra

Kwa kweli wazungu wa zama za kale hawakukosea waliposema kuwa kucheka ndio dawa bora.

Basi leo siku ambayo wakazi wa Kibra walikuwa wamengoja kwa hamu na ghamu, iliwadia na walijitokeza kwa maelfu ili wakampigie kura mgombea wa kiti hicho cha Kibra, wanayemu enzi.

Basi baadhi ya wana Kibra waliojitokeza walikuwa na mavazi na mitindo ya kipekee ambayo kwa uhakika yalivunja baadhi ya shingo katika maeneo hayo ya kupigia kura.

Jamaa mmoja aliwashtua wengi alipovalia suruali refu ajabu ambayo ilikuwa imefungiwa kifuani kinyume na kawaida yake, ambapo ni kiunoni.

Tazama picha zifuatazo.