Makosa aliyofanya MacDonald Mariga, angembwaga Imran Okoth

untitled_design_-_2019-09-25t175205.784
untitled_design_-_2019-09-25t175205.784
Baada ya tume ya IEBC kumtangaza Imran Okoth wa ODM kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Kibra, sababu zinaonekana wazi ni kwa nini staa wa soka MacDonald Mariga alipoteza nafasi hiyo.

Nduguye Ken Okoth alipata kura elfu 24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Sababu ya kwanza kumuangusha ni chama chake.

Eneo la ubunge la Kibra ni ngome ya ODM kwa miaka mingi zaidi.

Kuuza mgombeaji wa Jubilee Kibra ni ndoto ya mchana.

Pili, Mariga hana ukomavu wa kutumia lugha ya Kiswahili na Kizungu.

Katika hotuba alizozitoa katika mikutano mbalimbali ya kisiasa, Kiswahili chake pamoja na kizungu zilimfedhehesha.

Kwa kiongozi yeyote anayetaka kushawishi wapiga kura, lazima awe na uwezo wa kuhutubia raia ipasavyo.

Mariga alijaribu kuchanganya ndimi.

Sio kizungu sio Kiswahili sio sheng, Mariga angechagua lugha moja ya kutumia na hivyo manifesto yake ingefikia wananchi vyema.

Tatu, Mariga hajawahi kuwa na ndoto ya kuzamia siasa wala hana ujuzi wa kuendesha kampeni.

Ina maana ata huenda manifesto yake aliandikiwa na 'mtu' aliyekuwa na ndoto za Kibra akilini.

Mwisho, MacDonald Mariga hakuwa na kura. Aidha, waliompigia debe hawakuwa na kura ya kumpigia. Ruto , Duale na wengineo hawakuwa wa msaada mkubwa kwake.

Kikosi cha Imran kilijihami na kura akiwemo baba Raila Odinga.

Huenda Mariga hajawahi piga kura maishani mwake.