Toboa Siri! Mashabiki wamtaka Kate Actress afichue baba ya mtoto wake

Screenshot.from.2019.11.13.10.20.57
Screenshot.from.2019.11.13.10.20.57
Catherine Kamau ajulikanaye kama Kate Actress, ana mimba ya mtoto wa pili na baba ya mtoto huyu ni mume wake bwana Phil Karanja.

Wapenzi hawa wamekaa pamoja katika uhusiano mzuri na ni wazi kuwa wawili hawa wanapendana sana.

https://www.instagram.com/p/B3q2tLcnibF/

Wawili hawa hawajakuwa wakificha kitu chochote kuhusu mapenzi yao isipokuwa jina la baba ya mtoto wa kwanza wa Kate Actress.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, Kate Actress aliulizwa na shabiki mmoja kama baba ya mtoto wake wa kwanza amewahi rudi katika maisha yao na ilikuwa ni wazi kuwa jamaa huyu hajawahi rudi katika maisha yake Kate na mtoto wake.

https://www.instagram.com/p/B4JuTErHYyh/

Kate Aliulizwa swali na akajibu akiwa na mori sana kuwa bwana huyu hajawahi rudi.

Resurfaced from where? Kate Alisema.

Pindi tu baada ya swali lile, Kate aligeuza mazungumzo na ikawa wazi kuwa kidosho Kate hakutaka kuzungumzia kilichotendeka.

Hivyo basi mashabiki wamekuwa na maswali mengi sana na wanatamani sana kujua baba ya mtoto wake wa kwanza wa Kate.