Mkondo tofauti wa hekaya za Paul Manyasi, DCI yatoa kauli inayokanganya zaidi

Screenshot_from_2019_11_17_10_26_55__1573975660_52818
Screenshot_from_2019_11_17_10_26_55__1573975660_52818
Hekaya za kijana aliyeanguka kutoka kwa ndege nchini Uingereza zinachukua mkondo tofauti siku baada ya siku.

Kwa kile kinachoonekana kama uchunguzi uliogonga mwamba, ofisi ya DCI imetoa kauli kinzani na shirika la habari la Sky News.

Mkuu wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Bwana Kinoti amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa kijana aliyefariki katika ndege ya KQ ,Paul Manyasi ana uraia wa Afrika Kusini.

Katika mahojiano na kituo cha K24, Kinoti amefunguka A-Z kuhusu swala hilo.

"Tungetaka kujua habari zote zinazozingira tukio hili. Aidha ni muhimu tujue kizungumkuti hiki chote kimesababishwa na nini. Tutajitahidi kuona iwapo kijana aliyeanguka kutoka kwa ndege ana uraia wa Kenya ama ni Afrika Kusini..." Kinoti

Kinoti amesema kuwa safari ya ndege hii ilianzia Afrika Kusini kabla itue JKIA.

Taarifa za DCI zinakanganya kwani angepanda ndege Afrika Kusini, mwili wake ungeanguka Kenya punde tu magurudumu yakichomoka.

Wazo la kufikiria kuwa kijana huyu ni raia wa Afrika kusini ni wazo la kupuuzilia mbali.

Haya yanajiri huku sura ya picha iliyochapishwa na Sky News ikifanana na kijana kwa jina Cedric Sivonje.

Inadaiwa kuwa Shivonje amezuiliwa katika jela kwa tuhuma za ubakaji.

Hii ni kulingana na makachero wanaochunguza kisa hiki.

Idara ya DCI imezidisha juhudi Afrika Kusini kubaini kisa hicho na kudadisi uwezekano wa marehemu kutoka nchi hiyo.

Shirika la habari la Sky News linashikilia kuwa Paul Manyasi ndiye alifariki katika ndege ya KQ.

Ripota wa shirika hili alisafiri hadi Kenya,Kakamega kumhoji anayedhaniwa 'babake'.

'Wazazi' hawa Isaac Beti na Janet walikubali na baadaye wakageuka baada ya kuona habari hizi katika vyombo vya habari.