Wakili maarufu Mombasa ajiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya 10

Wakili mmoja maarufu jijini Mombasa amejiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya 10 kwenye jengo la serikali.

Jamaa huyo alitambulika kuwa Sammy Anyazwa mwenye umri wa miaka 69, alifariki Jumatano baada ya kuruka kupitia dirisha la jengo hilo refu Mombasa.

Afisa mkuu wa polisi OCPD Eliud Arumbi amethibitisha tukio hilo lililotokea adhuhuri.

Arumbi amesema kwamba chanzo cha wakili huyo kujiua kingali kubainika.

Aidha wafanya kazi wenzake wanasema mwendazake hakuonesha dalili zozote za msongo wa mawazo au masumbufu yoyote.

Alithibitishwa kufariki alipofikishwa katika hospitali ya Pandya, ambako alikimbizwa na wasamaria wema kwa matibabu ya haraka.

Hatimaye mwili wake ukapelekwa katka chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.

Soma taarifa nyingine kutoka mwaandishi: